
Ndugu zangu,
Ninapomsikiliza
Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye kwenye taarifa yake inayotokana na
kikao cha Kamati Kuu, Kisiwandui, naipata tafsiri moja kuu; kuwa CCM
imebaini, kuwa ' Bahari Ya Kisiasa Imechafuka'.
Wimbi la
Escrow ni kubwa mno kwa CCM kulidhibiti kuelekea Uchaguzi Mkuu. CCM
inataka kulikwepa. Inataka kwenda kwenye uchaguzi ikiwa na sahani safi
na kavu- Not only a clean slate, but a dry one.
Hivyo,
CCM haina namna yeyote, bali kuwaacha wote wenye kuhusishwa na Escrow
waogelee wenyewe bila kutegemea maboya ya chama. Katika hili, na kwa
kupitia taarifa ile ya Nape Nnauye, Waziri wa Nishati na Madini,
Sospeter Muhongo ametoswa rasmi.
Yawezekana
kabisa kuwa Sospeter Muhongo amefanya kazi njema kwa taifa kupitia
Wizara yake, lakini, maisha ya kisiasa ni magumu. Hapa hesabu za kisiasa
zinamtaka aondoke, kwa kujiuzuru mwenyewe, au kusubiri kuwekwa kando na
aliyemteua. Na maisha ya kisiasa yataendelea. Muhongo anaweza kurudi
tena kwa nguvu zake mwenyewe.
Maggid ,Dar es Salaam


No comments:
Post a Comment