Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na wajumbe wa Jopo la
Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN
Independent Review Panel) linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana
Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae ( aliyekaa wa kwanza kulia kwa Rais
Kikwete) huko Ikulu jana.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Results
Now kwa Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae
aliyeongoza jopo maalum la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo
Makubwa Sasa
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Result
Now kwa Dkt. Sipho Moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ONE wa Kanda ya Afrika
aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa jopo la kutathmini Programu ya
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa. Rais Kikwete aliwakabidhi tuzo hizo
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi Tuzo Maalum ya Vision 2025 Big Results
Now kwa Bwana James Adams, Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia
aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakipiga picha ya pamoja na
wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa
Sasa (BRN Independent Review Panel). Kulia kwa Mheshimiwa Rais Kikwete
ni Rais Mstaafu wa Botswana Dkt. Festus Mogae akifuatiwa na Bwana James
Adams (Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia), aliyesimama wa kwanza
kushoto ni Bibi Linah Mohohlo (Gavana wa Benki Kuu ya Botswana) na wa
kwanza kulia ni Dkt. Sipho Moyo (Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika,
ONE. Waliosimama mstari wa nyuma (kulia kwenda kushoto) Dkt. Nkosana
Moyo (Mwanzilishi wa Mandela Institute for Development Studies)
akifuatiwa na Lord Peter Mandelson (Mwenyekiti, Global Counsel
‘Uingereza’), anayefuata ni Bwana Knut Kjaer, (Mwenyekiti, Trident Asset
Management, ‘Norway’). (Picha zote na John Lukuwi)


No comments:
Post a Comment