Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, akisalimiana
na Mbunge wa Jimbo la Rahaleo Mhe Abdalla Juma Mabodi, alipofika katika
jimbo hilo kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama na kujionea
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi yaCCM kwa Wananchi wa Jimbo hilo.
(Picha zote kwa hisani ya ZanziNews)
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana,
akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo, Mhe Nassor Salim
Jazira, alipowasili katika Tawi la CCM Makadara chini,kuangalia
utekelezaji wa Ahadi za Mbunge na Mwakilishi kwa Wanachi wa jimbo hilo
na kuzindua mradi wa utandazaji wa mipira ya kusambazia maji kwa
wananchi wa Shehia ya Makadara chini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akisalimiana
na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo alipowasili katika Tawi la CCM Makadara
Chini, akiwa katika ziara yake kutembelea miradi na kuimarisha Chama na
kujionea utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa wananchi wake.


No comments:
Post a Comment