
Real
Madrid, mabingwa mara kumi wa Ulaya, wameweza kushikilia nafasi ya
kwanza kama timu tajiri zaidi duniani kwa mwaka wa kumi mfululizo,
katika orodha ya Deloitte ya timu tajiri duniani.
Manchester
United imesogea hadi nafasi ya pili kutoka ya nne, katika tathmini
iliyofanywa kwa kuzingatia mapato ya msimu wa 2013-14.
Bayern Munich, Barcelona na Paris Saint-Germain zimechukua nafasi ya tatu, nne na tano.
Klabu
za England za Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool zimo
katika nafasi kuanzia sita hadi tisa, zote zikionesha ongezeko zuri la
mapato.
Orodha kamili ya kumi bora pamoja na mapato msimu wa 2013-14 ni kama ifuatavyo kwa sarafu ya Euro:
(Kwenye mabano ni mapato ya msimu wa 2012-13)
1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)
2. Man Utd: 518m (423.8m)
3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)
4. Barcelona: 484.6m (482.6m)
5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)
6. Manchester City: 414.4m (316.2m)
7. Chelsea: 387.9m (303.4m)
8. Arsenal: 359.3m (284.3)
9. Liverpool: 305.9m (240.6m)
10. Juventus: 279.4m (272.4m)


No comments:
Post a Comment