![]() |
| Hapa akiapishwa na wananchi |
Wakati Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani-Segerea, Dar es Salaam,
Japhet Kembo, aliyejiapisha kwa kutumia wakili binafsi akiapishwa tena
jana na wakili aliyechaguliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameonya vitendo vya
wadau wa siasa kujichulia sheria mikononi na kuwataka wafuate sheria na
taratibu.
Kembo aliyejiapisha mwanzoni mwa wiki hii,
alijumuika na wenzake kutoka mitaa ya Migombani - Kiwalani na Kigogo
Fresh B katika tukio lililoshuhudia mwenyekiti mteule wa Kigogo
akishambuliwa na wafuasi wa Ukawa na kuzuia uapishwaji wake. Baada ya
kuapishwa, Kembo alisema sasa yupo rasmi kwa ajili ya kuwatumikia
wananchi wake waliomchagua kwani siku zote alikuwa na shauku ya kuingia
ofisini kuanza kazi.
Wakati hilo likikamilika, wafuasi wa Ukawa
walimshambulia na kuzuia kuapishwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Fresh B,
Mariano Maurus wa CCM kwa madai kuwa hakushinda nafasi hiyo.
Mwenyekiti huyo aliachwa kiporo kutokana na utata
wa matokeo kwenye uapishaji wa wajumbe wa Manispaa ya Ilala. Wakati
akishambuliwa na kuondolewa eneo la tukio, aliwaacha wenyeviti wenzake
wawili; Kembo na Ubaya Chuma wa Migombani - Kiwalani wakikamilisha
mchakato huo pamoja na wajumbe 15 wa mitaa yote mitatu.
Mwanasheria wa manispaa hiyo, Mashauri Musimu
alisema pamoja na yote yaliyotokea kwa mwenyekiti huyo, Maurus ndiye
anayetambulika kutokana na kumbukumbu za matokeo zilizopo hivyo lazima
ataapishwa ili awatumikie wananchi.
Shambulizi hilo lilitokea jana asubuhi wakati
wajumbe wakiitwa kuingia ukumbini na lilipoitwa jina Maurus
alishambuliwa na baadhi ya makada waliokuwapo eneo hilo kabla askari
hawajamwokoa, akiwa ameshachaniwa nguo.
Jaji Mutungi
Akizungumzia tukio la kujiapisha, Jaji Mutungi
alisema ingawa kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mtaa zinampa mamlaka
wakili, hakimu wa Mahakama ya Mwanzo na ya wilaya kuwaapisha viongozi
waliochaguliwa, kuna utaratibu ambao lazima ufuatwe.



No comments:
Post a Comment