KIKAO
cha pamoja kilichowakutanisha viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), kimetoa mikakati ya pamoja ikiwamo kuandaa ratiba ya uteuzi wa
wagombea wa nafasi ya urais kwa kila chama.
Hatua hiyo imekuja baada ya kikao cha siri cha siku mbili kilichowakutanisha viongozi wa juu wa Ukawa ambao ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Dk. Emmanuel Makaidi (NLD).
Chanzo cha kuaminika kiliambia MTANZANIA jana kuwa katika kikao hicho, viongozi hao wamekubaliana kuweka mikakati hiyo ikiwamo ya kushika dola katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Katika kikao hicho, viongozi hao wametoa ratiba ambayo inakitaka kila chama kuteua mgombea wake wa urais ili ajulikane mapema kabla vikao vya Ukawa kuteua jina la mgombea mmoja.
“Imewekwa mikakati hii kwa lengo la kuimarisha demokrasia kwa kila chama husika, hasa vinavyounda Ukawa vipate muda wa kutosha wa kuweza kufanya uteuzi mapema.
“Lakini pia sasa ni wakati kwa wale wazalendo wa kweli, hasa kutoka upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wana uchungu na nchi yao wajitoe mapema na kuja kushiriki uchaguzi kupitia Ukawa badala ya kusubiri hadi mwisho, kwani wakifanya hivyo wanaweza wakakuta milango imefungwa.
“Hili linaweza kuwafanya washindwe kupata nafasi sasa, maana ni wazi Ukawa ndiyo tegemeo la Watanzania wengi kwa sasa ambao wapo tayari kukabidhi dola katika uchaguzi ujao,” kilisema chanzo hicho.
Mbali na kuweka mkakati hiyo, viongozi hao wa Ukawa wameandaa kanuni za uchaguzi ambazo kila chama kinatakiwa kuwasilisha katika vikao vyake vya uamuzi na kuweza kujadili kama njia ya kushika dola.
Mikakati hiyo ya Ukawa inatarajiwa kuwekwa wazi leo ambapo wenyeviti wote wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari.MTANZANIA

No comments:
Post a Comment