Mkutano wa wakuu wa Nchi za Umoja wa
Afrika unaanza leo nchini Ethiopia ambapo viongozi wa Afrika
wanatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayolikumba bara la Afrika kwa
sasa.
Baadhi ya maswala yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo
niharakati za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, pamoja na juhudi za
kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Licha ya kauli mbiu ya
mkutano huo wa siku mbili kuwa swala la kuwawezesha wanawake, viongozi
kutoka nchi 54 wanachama wa Muungano huo watalazimika kangazia swala la
migogoro ambalo limekluwa changamoto kubwa kwa bara la Afrika.
Mwenyekiti
wa muungano huo, Nkosazana Dlamini-Zuma amepigia debe swala la umoja
katika kupambana na wapiganaji wa kiisilamu wanaoendelea kuteteresha
amani katika bara hilo.
Mnamo siku ya Alhamisi, baraza la usalama
na amani la AU, lilitoa wito wa haja ya kuwepo kikosi cha wanjeshi 7,500
kupelekwa katika maeneo yanayokumbwa na migogoro Afrika.
Wakati
huo huo Kenya inatarajia kutuma ujumbe mzito kwenye mkutano huo kama
mwanzo wa hatua yake ya kukata uhusiano na Mahakama ya jinai ICC.
Katika
kikao kilichopita cha Umoja wa Afrika kilichokaa mjini Malabo
Equatorial Guinea wajumbe walisaini mkataba wa uundwaji wa mahakama ya
Afrika itakayoshughulikia kesi za Afrika badala ya kuzipeleka kwenye
mahakama ya ICC, baadhi yao wakidai kuwa kesi za mahakama hiyo
zinawalenga waafrika pekee



No comments:
Post a Comment