Msimamizi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao aliyesimama
(kushoto)akionyeshwa namba ya mmoja wa washindi na Meneja Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) wakati wa kuchezesha
droo ya nne ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo
iliyofanyika mwishoni mwa wiki, wengine katika picha (kulia) ni mtaalamu
wa mifumo ya kompyuta Michael Kanakakis, waliokaa (kutoka kulia) ni
Dimitrios Lintis na Zakaria Kanyi. Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Msimamizi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao (kulia)akihakiki namba
ya mmoja ya washindi toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom
Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) wakati wa kuchezesha droo ya nne ya
Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni
moja kila mmoja. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno
Jay kwenda 15544.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto)
akiwasiliana na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo ya nne ya
Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni
moja kila mmoja. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno
Jay kwenda 15544. Kushoto kwake ni msimamizi wa bodi ya michezo ya
kubahatisha Mrisho Millao.
Dar es Salaam Januari 18,2015:Wateja watano wa Vodacom Tanzania
wamejishindia milioni 1 kila mmoja wao katika droo ya tatu na ya nne ya
promosheni ya Jaymillions iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Washindi hao ni Janeth Peter Nganyange,mjasiriamali na mkazi wa
Njombe,Stanley Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya
sekondari ya Ibizamanta,Evarista Minja mkazi wa Mwanza na mwanafunzi wa
mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine,
Ramadhan Hamis Maulid mkazi wa Dodoma ambaye ni mkulima na Walter Minja
ambaye ni Dalali.
“Nimefurahi sana kwa kushinda milioni 1 kupitia promosheni ya
Jaymillions kwa kuwa kwa kiasi kikubwa fedha hizi zitanisaidia kupanua
biashara yangu na kununulia watoto wangu mahitaji mbalimbali”.Anasema
Janeth Peter Nganyange (40) mkazi wa Njombe mmoja wa washindi.
Nganyange amesema ushindi huu umeleta faraja kubwa kwake na familia
yake ikizingatiwa kwamba miezi mitatu iliyopita alifiwa na mme wake na
kumuachia familia yenye watoto wawili ambao anahangaika nao kuwalea.
“Mungu ni mkubwa na ushindi huu umeleta faraja kubwa kwangu na nashukuru
Vodacom kwa kubadilisha maisha yangu kwa maana kwa muda mrefu nilikuwa
nahangaika kutafuta mkopo wa kuendeleza biashara yangu bila
mafanikio”,Anasema.
Mteja mwingine aliyejishindia milioni ni Walter Minja,mkazi wa Mbezi
beach jijini Dar es Salaam ambaye ni mwajiriwa ambaye pia amesema kuwa
amefurahia kuibuka mshindi hasa katika kipindi hiki cha mwezi wa kwanza
ambao unakuwa ni mgumu kwa watu wengi.
“Nafurahi kujishindia milioni moja ya Jaymillions na itanisaidia sana
kuvuka katika mwezi huu mgumu wa Januari ambao unakuwa na mambo
mengi.Nashukuru Vodacom kuandaa promosheni hii na nawahimiza watanzania
wenzangu kushiriki kwa kucheki namba zao za simu kama zimeshinda
“.Amesema Minja.
Stanley Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya
sekondari ya Ibizamanta amesema amefurahi kupata ushindi na fedha hizo
zitamsaidia kutimiza ndoto yake ya muda mrefu wa kufungua duka la M-Pesa
“Fedha hizi zimekuja wakati muafaka naamini ndoto yangu ya kufungua
duka la M-pesa imetimia”.Alisema.
Mshindi mwingine Evarista Amedeus Minja mwanafunzi wa mwaka wa nne wa
sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine amesema amefurahia
kujishindia milioni 1/- za Promosheni ya Jaymillions na zitamsaidia
kukamilisha masomo yake. “Fedha hizi zimepatikana katika wakati mwafaka
na zitanisaidia kulipia gharama za hosteli na kumalizia utafiti wangu
kwa kuwa sipati mkopo kutoka Bodi ya Mikopo”.Alisema kwa furaha.
Naye Ramadhan Maulid alisema amefurahia ushindi huu na fedha hizo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo “Nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii na nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kushiriki “.alisema.
Naye Ramadhan Maulid alisema amefurahia ushindi huu na fedha hizo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo “Nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii na nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kushiriki “.alisema.
Mbali na washindi hao wa fedha taslim wateja wengi wamejishindia muda wa maongezi.
Kwa upande wake ,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom
Tanzania Rosalynn Mworia amewapongeza washindi na kuwahimiza wateja wote
wa Vodacom kuangalia namba zao kila siku kama zimeshinda kwa kutuma
ujumbe mfupi wenye neno JAY kwenda namba 15544 ili wasipoteze nafasi
zao za kushinda.
“Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions itakayofanyika kwa siku
100 mfululizo inawahusisha wateja wote wa Vodacom ,kiasi kikubwa cha
fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara
tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha
kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na
kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/-
tu”.Alisema.
Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa
Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia
moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye
thamani ya Sh. 1000/-


No comments:
Post a Comment