KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 26, 2015

YANGA NA KASEJA KUTOKA UWANJANI HADI MAHAKAMANI

Yanga imemburuza mahakamani mlinda mlango wao, Juma Kaseja wakitaka awalipe Sh340 milioni ikiwani fidia.
Yanga wamefikia uamuzi huo Ijumaa iliyopita baada ya kufikisha kesi Mahakama ya Kazi na tayari Kaseja ameshapewa notisi ya kuitwa mahakamani kujibu shtaka la kukacha timu yake  ikiwa ni pamoja na kulipa kiasi hicho cha fedha.
Yanga wanataka Kaseja awalipe Sh340 milioni ikiwa ni ada ya usajili, ambayo ni Sh40 milioni pamoja na fidia ya Sh300 milioni ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga.
Mmoja wa viongozi wa Yanga aliliambia gazeti hili kuwa kuna nyaraka ambazo Yanga wanatakiwa kuzikamilisha ili wapangiwe hakimu wa kusikiliza kesi hiyo ambayo itafungua ukurusa mpya wa bifu na kisasi miongoni mwa Yanga na mlinda mlango huyo.
Wakili wa Yanga, Frank Chacha alikiri klabu hiyo tayari imeshamfungulia mashtaka Kaseja na kesho wanategemea kupangiwa hakimu wa kusikiliza shauri hilo.
Kaseja aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya Novemba 11 mwaka jana kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kukiuka makubaliano ya mkataba kati yao akishinikiza kulipwa Sh20 milioni za usajili alizokuwa anaidai klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment