KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 26, 2015

ZITTO:HATA KAMA PROF.MUHONGO KAJIUZULU, SERIKALI IMETEKELEZA MAAZIMIO YA BUNGE KWA ASILIMI 35 TU


 

Zitto_Kabwe_2011
Fredy Azzah na Nora Damian, Dar es Salaam
SIKU moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kutangaza kujiuzulu kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema suala hilo bado ni bichi.
Pamoja na hali hiyo, PAC imesema hadi sasa Serikali imetekeleza maazimio manane ya Bunge kwa asilimia 35.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, alisema kati ya maazimio manane yaliyopitishwa na Bunge hadi sasa ni matatu pekee yaliyotekelezwa.
Alisema suala la Akaunti ya Tegeta Escrow ni kubwa kuliko Profesa Muhongo, hivyo watu waliodhani kuondoka kwake litakuwa mwisho wanajidanganya.
“PAC itaendelea kupaza sauti ili maazimio yatekelezwe. Watu waliodhani kuwa akitoka (Profesa) Muhongo basi suala hili limekwisha wanajidanganya. Suala hili ni kubwa zaidi ya Muhongo,” alisema Zitto.
Maazimio nane ya Bunge
Akifafanua maazimio yaliyopitishwa na Bunge, Zitto alisema la kwanza lilikuwa linamuhusu Singh Seth (Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme ya Pan African Power Limited (PAP) na watu wengine waliotajwa na taarifa ya PAC.
Azimio hilo lilitaka watu hao kuchukuliwa hatua na vyombo vya sheria kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusika katika vitendo vya jinai. Zitto alisema mpaka sasa ni vidagaa tu wamefikishwa mahakamani kuhusiana na suala hilo.
“Waliofikishwa mahakamani ni wapokeaji tu na sio watoaji, waliopewa fedha kupitia Stanbic hatujawaona mahakamani.

No comments:

Post a Comment