Mfuko wa Pensheni wa GEPF umesaini mkataba wa uwekezaji na
Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika eneo la Bunju. Uwekezaji
huo utakaohusisha kumbi za mikutano (Conference Halls) zenye uwezo wa
kuchukua watu Zaidi ya 1,200, migahawa (Restaurants), Hoteli yenye
hadhi ya kimataifa yenye vyumba Zaidi ya 102, Maktaba, Bwawa la
kuogelea (Swimming Pool) pamoja na sehemu za mazoezi (Gymnasium)
Uwekezaji huo utagharimu Zaidi ya shilingi Bilioni 10 za kitanzania na
unategemewa kukamilika katikati ya mwaka huu 2015.
Mkurugenzi
Mkuu wa GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia) akiongoza majadiliano ya
awali kati ya Menejimenti ya GEPF pamoja na Menejimenti ya NBAA kabla
ya zoezi la kutiliana saini mkataba wa uwekezaji.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GEPF,Bi. Joyce Shaidi (kulia) pamoja na mwenyekiti wa NBAA
Profesa Issaya Jairo wakisaini mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji wa
pamoja wakiongozwa na mwanasheria wa NBAA Bi Agness Kessy.
Utiaji
saini huo ulishuhudiwa na makamu mwenyekiti wa NBAA Bi Anna Mbughuni (
mwenye suti ya blue), Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Bw Pius Maneno,
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi pamoja na Mkurugenzi wa
Uwekezaji wa GEPF Bw Festo Fute.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GEPF Bi Joyce Shaidi akibadilishana nyaraka za mkataba wa
uwekezaji wa pamoja na Mwenyekiti wa NBAA Profesa Issaya Jairo.
Pichani baadhi ya watendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) wakifurahia jambo mara baada ya zoezi hilo kukamilika.


No comments:
Post a Comment