
Aliyekuwa
mkuu wa shirika la fedha duniani IMF,Dominique Strauss Kahn ameshtakiwa
nchini Ufaransa na mashtaka ya usaidizi wa kuwanunua wanawake ili
kushiriki katika sherehe za ngono.
Bwana
Straus Kahn ambaye alitabiriwa kushinda uchaguzi wa urais nchini
Ufaransa alilazimika kukata harakati zake za kisiasa baada ya kudaiwa
kum'baka msichana mmoja msaidizi.

Ameshtakiwa kwa kuwa katikati ya mtandao wa ukahaba mjini Paris,Brussels na Washington.
Bwana Straus-Kahn amekana kujua kwamba wanawake katika sherehe hiyo walilipwa.
Straus
Kahn na mwanamke msaidizi ambaye alidai kunyanyaswa kijinsia na
KahnMwandishi wa BBC mjini Paris amesema kuwa kesi hiyo ni jaribio la
kubadilisha mitazamo ya kimaadili nchini Ufaransa.


No comments:
Post a Comment