Wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi wakimsikiliza kwa makini mwalimu wa masuala ya Afya na Uzazi wa Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi, mpango huu uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara |
Wasichana kutoka kata ya Ufukoni mkoani Mtwara wakisubiri kupatiwa pedi kwa ajili ya kujisitili kipindi wakiwa kwenye hedhi na kupatiwa elimu ya Afya na uzazi chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation.Mradi huo unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wale wasio mashuleni ambapo zoezi hili limeanza kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara. |
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi
wakifurahia baada ya kugawia pedi za kujikinga
wanapokuwa kwenye hedhi .Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na
kuwapatia elimu ya Afya na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna
Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na
Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni
na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyanyika katika mikoa ya
Lindi na Mtwara.
“Sasa nafurahia masomo yangu ikiwemo maendeleo yangu darasani kuwa mazuri darasani.Najisikia vizuri
kuwa mwanafunzi.Natamani mradi wa
Hakuna Wasichoweza ungeanza kitambo.Hata hivyo naona mabadiliko
makubwa ya kumuwezesha mtoto wa kike na kumjengea uwezo wa kujiamini
yanakuja tukiendelea na kasi hii…”Haya yalisemwa na Sharifa Hamis,
mmoja wa wanafunzi wa sekondari mkoani ya msingi
ya Mwenge iliyopo mkoani Mtwara wakati akitoa ushuhuda kwa niaba ya
wenzake ni kwa jinsi gani wasichana wenzake zaidi ya 5,000 wamenufaika
na mradi alipohojiwa hivi karibuni.
Mwanafunzi Sharifa alikiri kuwa tangu kuanzishwa kwa mradi wa
Hakuna Wasichoweza maarufu kama
Girl Power mahudhurio ya wasichana shuleni kipindi
chote cha masomo yameongezeka pia ufanisi wao katika masomo umeongezeka
kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.Ushuhuda huo uliungwa
mkono na mwalimu Masoud Issa anayefundisha
katika shule hiyo.
Baada
ya kupatiwa mafunzo ya Afya na mafunzo kuhusiana na mabadiliko ya
miili yao ikiwemo kuwapatia pedi wasichana wanaotoka katika familia
maskini
kwa ajili ya kujihifadhi wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi wasichana
wengi wameanza kujiamini na kupunguza utoro wa kuja shuleni
uliosababishwa na hali hiyo kutokana na shule wanazosoma kutokuwa na
mazingira rafiki ya kujihifadhi katika kipindi hicho.
Mafunzo
kwa wasichana na namna na kujihifadhi wakati wakiwa hedhi pamoja na
afya ya uzazi yanafanyika chini ya uwezeshaji wa walimu na
wauguzi waliopewa mafunzo hayo. Kitini cha kufundishia juu ya masuala
haya kimeweza kuandaliwa na taasisi ya T-MARC kwa kushirikiana na
Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia mradi huu wa ‘Hakuna
Wasichoweza’ na kina maelezo ya kina juu ya umuhimu wa afya,elimu ya uzazi na matumizi ya Pedi.
Mmoja
wa walimu wanaotoa mafunzo kwa wasichana Monica Mfaume,anasema kuwa
mradi huu umeleta mabadiliko makubwa katika kipindi cha muda
mfupi tangu uanze na aliwapongeza waliounzisha na kuwaomba waufanye
kuwa endelevu na usambae nchi nzima na kuwafikia wasichana wengi zaidi.
“Tatizo la mahudhurio hafifu ya wasichana na kufanya vibaya katika
masomo ikiwemo kupata mimba katika umri mdogo kutokana na kutojua
mabadiliko katika makuzi yao lilikuwa linatuvunja moyo lakini angalau
hivi sasa linapungua kwa kasi eneo hili la mradi ”.Alisema
Meneja
Uhusiano wa taasisi ya T-MARC inayotekeleza mradi chini ya ufadhili wa
USAID na Vodacom Foundation,Maurice Chirimi, anasema kuwa
mradi umeonyesha kuwa na mafanikio kwa muda mfupi wa miaka 2 ya awamu
ya kwanza kwa
mafunzo
pamoja na pedi za bure kuwafikia wasichana zaidi ya 5,232 waliopo
katika shule 24 za msingi na wengine 552 wasiokuwepo mashuleni katika
kata 17 mkoani Mtwara.
Lengo la Mradi wa
Hakuna Wasichoweza ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea
uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi watoto wa kike zaidi ya wasichana
10,000 waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mikoa ya Mtwara na
Lindi.Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo
wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa
na wenzao wa kiume.
Nia ya
Hakuna Wasichoweza ni kuwaona walimu ,watoto wa kike na
wanajamii kwa ujumla ikiwemo wanaharakati wa masuala ya elimu wakiunga
mkono juhudi hizi ili kwa pamoja tuifikie dira ya maendeleo ya Taifa ya
mwaka 2015.Elimu
Bora bila ubaguzi inawezekana,Timiza wajibu wako. |
No comments:
Post a Comment