![]() |
Jide
akiwa na Mokonyo (mtoto wa mdogo wake Dabo)Lady Jaydee ameendelea
kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine
aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye
huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa
kupitia EATV. “SWALI: Una watoto wangapi?JIBU : Sina mtoto wala watoto SWALI:Utazaa lini?JIBU : Sijajua mpka sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa. SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao. SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ?Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeyeAnaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /MusomaJIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11 Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia. SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”. |
February 19, 2015
LADY JAY DEE AFUNGUKA KUHUSU KUWA NA MTOTO!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment