Mbunge
wa Ileje Mheshimiwa Aliko Kibona akimkaribisha Waziri wa Ujenzi
Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kabla ya ukaguzi wa daraja hilo la mto
Songwe.kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Rosemary Sitaki Sinyamule.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa barabara ya Isongole-Itumba km 9 katika Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.
Kulia ni Mbunge wa Ileje Mheshimiwa Aliko Kibona. Wengine ni Mkuu wa
Wilaya ya Ileje Bi Rosemary Sitaki Sinyamule, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi Eng. Musa Iyombe pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara
nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale.
Wakazi
wa Ileje wakishangilia mara baada ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli kuahidi ujenzi wa Barabara ya Mpemba-Isongole km 58 kwa
kiwango cha lami.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) Eng. Consolatha Ngimbwa
akizungumza kuhusu usimamizi makini wa Bodi yake kwa Makandarasi kabla
ya Waziri wa Ujenzi kuhutubia mamia ya wakazi wa Ileje.


No comments:
Post a Comment