KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 19, 2015

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AFUNGUA RASMI MKUTANO WA KIKANDA JUU YA UKUAJI NA MAISHA YA BAADAE YA MIJI YA AFRIKA MASHARIKI

1
Afisa mtendaji mkuu waTaasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) Prof.Joseph Semboja, (Kulia) akimkaribisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh. Balozi Seif Ali Iddi, (kushoto) kufungua rasmi Mkutano wa kikanda uliokutanisha viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika mashariki , kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika mpaka ifikapo 2050, katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel ya jijini Dar es Salaam.
2
Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) Prof. Joseph Semboja, (Kulia) akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh, Balozi Seif Ali Iddi, wa tatu toka kulia, kufungua rasmi mkutano wa kikanda uliokutanisha Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika mashariki , uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika mpaka ifikapo 2050, Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, na wa Pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia , mkutano huo wa siku mbili umefanyika leo katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment