| Paul Makonda |
DC Makonda, ameteuliwa kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni. Kiongozi huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM aliandikwa sana na vyombo vya habari wakati wa Bunge la Katiba kutokana na kutoa maneno ya kumshambulia mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba aliyewasilisha Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba.
Kiongozi
huyo wa UVCCM aliandikwa zaidi na vyombo vya habari kutokana na
kuhusishwa na vurugu zilizotokea Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es
Salaam wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa akidaiwa kumshambulia
mwilini Warioba, ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, makada wawili wa CCM, John Guninita na Mgana Msindai
walimwandikia kusudio la kumfungulia mashtaka wakidai kuwa Makonda
aliwadhalilisha kwa kuwaita kuwa vibara wa Edward Lowassa, ambaye ni
mbunge wa Monduli na aliwahi kuwa Waziri Mkuu.
Makonda
aliwahi kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtuhumu Lowassa
akidai kuwa anawatuma baadhi ya makada wa chama hicho wanaokivuruga
chama. Alidai kuwa Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania na kwamba CCM
haitafuti Rais pekee, bali mwenyekiti wake na mbunge huyo wa Monduli
hawezi kuongoza chama hicho kikongwe.Rais
Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya 12 na kuwateua
wengine 27, akiwamo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe
Stephen na mjumbe wa Bunge la Katiba, Paul Makonda ambaye aliingia
kwenye mzozo na mawaziri wakuu wawili wa zamani.
Katika
uteuzi huo uliotangazwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mjini hapa,
katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF), Frederick Mwakalebela
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, huku wakuu wa wilaya 64
wakibadilishiwa vituo vyao vya kazi.


No comments:
Post a Comment