![]() |
Mtu aliyebaguliwa na mashabiki wa Chelsea alilia haki
|
Mtu
aliyezuiliwa kuingia Paris Metro train na mashabiki wa timu ya mpira ya
Chelsea kwa sababu ya ubaguzi wa rangi ametaka waadhibiwe.
Mtu huyo mwenye miaka 33 anayeitwa Souleymane S aliambia gazeti la Le Parisien: “Hawa watu, hawa mashabiki wanapaswa kufungwa".
Video ilionyesha mtu huyo akizuiliwa kuingia kwenye Metro na akisukumwa na mashabiki hao.
Watu walisikika wakiimba: "Sisi ni wabaguzi wa rangi na hivyo ndivyo tupendavyo".
Kanda
hiyo ya video ilitolewa na gazeti la the Guardian lililotoa ripoti
kuwa tokeo hilo lilifanyika Richelieu-Drouot katika mji mkuu wa Fance
siku ya Jumanne kabla mechi ya Champions Legue.



No comments:
Post a Comment