![]() |
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO akikagua jengo lilokumbwa na ajali ya moto |
……………………………………………………………………………………………………
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema
Chiku Abwao alisikitishwa na uongozi wa shule ya sekondari ya Idodi
kushindwa kumpokea kama mbunge na mama aliyeguswa na ajali ya moto
katika shule kwa kuwa alikuwa ameshatoa taarifa kabla hajaenda katika
shule hiyo.
Kitendo
hicho kiliwafanya baadhi ya wanahabari wa manispaa ya Iringa waliokuwa
wameongozana na mbunge huyo kukasirishwa na kitendo kilichofanywa na
uongozi wa shule ya sekondari ya Idodi na walianza kuhoji je? angekuwa
mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya na waziri au mbunge wa jimbo hilo
wangemfanyia hivyo.
Licha
ya hujuma alizopewa ambazo zinasadikika kuwa za kisiasa mbunge wa viti
maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema
aliendelea na zoezi lake la kutoa msaada wa shilingi milioni moja ili
kusaidia majukumu mengine ya shule hiyo kutokana tathmini fupi
iliyotolewa na baadhi ya walimu.
Akizungumza
mbele ya wanafunzi wa shule Abwao amesema kuwa ameguswa na
ajali hiyo ya moto ndio maana ameamua kujitolea kutoa msaada huo.
Aidha ameishauri serikali kujenga mabweni kwa mtindo nyumba za kawaida
ili kuwawezesha wanafunzi kuishi kumi katika bweni moja tofauti na sasa
ambapo wanafunzi wanaishi zaidi ya mia na ishirini katika bweni moja.
Akasisitiza kuweka ulinzi mzuri kwenye mabweni kwa kuwa suala
kama hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika shule hiyo na
kuomba wakandarasi watakao kuwa wanapewa tenda za kujenga mabweni ya
shule kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kuzimia moto.
Alipotafutwa
mkuu wa shule kwa njia ya simu na kuulizwa kwanini amemkimbia mbunge
alijibu kuwa alikuwa na majukumu mengine kwa hiyo sio lazima
kumpokea mbunge na ninaweza kuwakilishwa kama kuna majukumu mengine
makubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment