| Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika
picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma
maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo
jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri
Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa
Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo
nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda
ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Kulia ni rafiki wa
mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, Swalah Saidi. Picha zote
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
No comments:
Post a Comment