| Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto),
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (watatu
kushoto), na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani.
Waziri Chikawe alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington
DC kujadiliana masuala mbalimbali likiwemo la Maafisa hao wakitarajia
kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji,
Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa
ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa
za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi
ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani.
Waziri Chikawe yupo jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa
Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa
kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
No comments:
Post a Comment