Bodi
ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,wataalam
wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti
kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi.
Mafunzo
hayo yalifunguliwa jana, na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Bw, Aziz
Kilonge, ambaye aliwaasa wataalam hao kuhakikisha kwamba wanasimamia
wanafunzi kwa ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti
zinazofanywa.
Aidha,
alifafanua kuwa uzingatiaji wa maadili katika kufanya tafiti, ndio
msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya
tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine
au kufanyiwa na watu wengine.
Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti, pia wanafunzi
wanajengewa uwezo wa kuandika ripoti na hata kuwasilisha ripoti katika
sehemu zao za kazi.
Hivyo lengo kuu ni kuwejengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa taifa.
Aliwakumbusha wasimamizi hao kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa
kujiamini na kujieleza kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo
wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi
atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
Mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akifungua mafunzo ya
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwa
kutoa mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya
ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya
stashahada ya ununuzi na ugavi mafunzo hayo yamefanyika kaktika ukumbi
baraza la Maaskofu TEC jijini Dar es salaam.
Tesha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence akizungumza katika mafunzo hayo mara baada ya kufunguliwa rasmi.
Mwezeshaji
wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr.Eli Tumsifu
akitoa mafunzo kwa wataalamu hao wa usimzmizi wa Manunuzi na Ugavi
Baadhi ya wataalamu wa Manunuzi na Ugavi wakifyuatilia mafunzo hayo. Wataalamu hao wakiandika mambo muhimu wakati wa mafunzo hayo. Mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akiwa katika picha ya
pamoja na wataalamu hao mara baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo.



No comments:
Post a Comment