KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 19, 2015

VIJANA KASULU WAPIGWA MSASA KUHUSU FURSA ZA MFUKO WA VIJANA

kas1
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga (watatu kutoka kulia kabla ya mabadiliko) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake leo. Kutoka kulia ni Afisa Utamaduni na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Mbogo, Afisa Vijana kutoka Wizara ya vijana Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa.
kas2
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofsini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba yao ya mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Bihigwe leo mjini Kasulu. Katikati ni Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa na wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana wa wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
kas3
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze (kushoto) akiagana na akipeana mkono na Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wakati walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa.

No comments:

Post a Comment