| Mkurugenzi Mtendaji waVodacom Tanzania Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. |
| Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. |
| Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia kwa makini hotuba
aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wao Rene Meza (hayupo pichani) kwa
waandishi wa habari juu ya mwenendo
wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Watanzania
wanaotumia huduma za mawasiliano bado wanaendelea kupata huduma hizo
kwa gharama nafuu kwa kupiga simu na matumizi ya interneti
ukilinganisha
na huduma zinazotozwa kupata mawasiliano katika nchi nyingine za Afrika
ikiwemo Afrika ya Kusini,Kenya,Nigeria na hata nchi ya india.
Haya
yaemebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene
Meza,katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo
alitoa
mfano kuwa licha ya ongezeko la bei katika vifurushi vya kupata huduma
mawasiliano bado katika kifurushi cha gharama ya chini ambayo ni
shilingi 500 mteja anaweza kupata MB za kutosha kutumia internet ikiwemo
kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS).
Alitoa
mfano kuwa mteja akinunua kifurushi cha shilingi 500,kati ya hizo fedha
shilingi 138 inakwenda serikalini kwa ajili ya kodi na kampuni
kubakia na shilingi 362/- ambapo fedha hizo zinamuwezesha kupata muda
wa dakika 15 za maongezi ikiwa kila dakika inatozwa shilingi 24/-,MB za
kuperuzi internet 8 kila MB ikiwa inatozwa shilingi 5 na kutuma ujumbe
wa maneno (SMS) 250 ambapo kila ujumbe natozwa
shilingi 0.12
“Viwango
vya malipo kwa Vodacom ni vya gharama nafuu na vimepangwa kulingana na
mahitaji ya wateja wetu licha ya mabadiliko madogo katika bei
yaliyofanywa hivi karibuni.Hivi sasa tunatoza shilingi 4.9/-kwa kila MB
katika kifurushi cha GB5 ambapo bei ya awali kilikuwa kinatozwa
shilingi 3.9/-.Bado malipo ya sasa ni madogo ukilinganisha na mallipo
yanayotozwa kwenye kifurushi cha GB5 kwenye soko
la huduma za mawasiliano kwa fedha za kitanzania kwa mfano Nigeria
inatoza shilingi 17/-/Afrika ya Kusini Shilingi 13/-,Kenya shilingi
12/-,Ghana shilingi 7/-na India shilingi 5/-
Meza
pia alielezea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na kampuni ya Vodacom
katika kipindi cha mwaka 2014 amabpo aliwashukuru wateja wote kuwa
wamechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo ikiwemo
zaidi ya wateja 1.7 kujiunga na familia ya Vodacom.
Pia
alisema kuna ongezeko la wateja wanaoendelea kufaidika na huduma
mbalimbali zinazotolewa na Vodacom ikiwemo huduma ya internet ya gharama
nafuu na huduma nyinginezo kama vile M-Pesa ambayo imekuwa na mafanikio
kwa kuwa na mtandao wa mawakala 85,000 na kufanya mihamala inayofikia
Trioni 1.2 kwa mwaka pia huduma ya M-Pawa imekuwa kwa kasi na
inawawezesha wateja wengi kuweka pesa na kukopa.Pia
aliongeza kuwa kampuni imeongoza kwa kuwa ya pili kulipa na kukusanya
kodi za serikali na kuwa ya kwanza katika sekta ya mawasiliano.
Alisema
kwa mwaka jana kampuni iliweza kuwekeza shilingi bilioni 180/- na
mwaka huu itawekeza shilingi bilioni 140/- katika kuboresha huduma
mbalimbali ikiwemo huduma ya internet na kusambaza huduma bora kwa
wateja nchini kote.
Alimalizia
kwa kusema kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kuunga mkono juhudi za
kusambaza huduma nchini kote hususani sehemu za vijijini ambapo
katika kuunga mkono jitihada hizi kampuni imekuwa ikichangia fedha
kwenye mfuko wa kusambaza huduma za mawasiliano vijijini ujulikanao kama
UCAF. |


No comments:
Post a Comment