KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 18, 2015

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI SINGAPORE

NHC1
Ujumbe wa NHC ulipokutana na baadhi ya wawekezaji wakubwa wa sekta ya uendelezaji Miliki wa Singapore ili kuwahamasisha kuwekeza vitega uchumi vya hoteli nchini Tanzania. Ujumbe huu umekutana na Bw. Henry Ngo ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bonvest na Hoteli ya Sheraton Singapore ambao pia wamewekeza Zanzibar Hoteli ya Kitalii
NHC2
Ujumbe wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi ukiwa katika Mamlaka ya Uendelezaji wa nchi ya Singapore(Urban Redevelopment Authority –URA) kujionea namna mamlaka hiyo inavyoratibu ukuaji wa sekta ya nyumba kwa kuweka mipango madhubuti ya matumizi bora ya ardhi kulingana na mahitaji ya Taifa hilo linalotegemea zaidi utalii.
NHC3
Mchoro unaoonyesha ramani ya nchi ya Singapore ulioko Makao Makuu ya Mamlaka ya Uendelezaji nchi hiyo ukionyesha majengo mbalimbali yaliyoko katika nchi hiyo yenye uhaba mkubwa wa ardhi.
NHC4
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia ramani yenye matumizi mbalimbali yaliyotengwa kwenye ardhi ya Taifa la Singapore. Katika nchi hiyo hakuna uwezekano wa mtu yeyote kuvamia kipande chochote cha ardhi kwa kuwa kila ardhi imepangiwa matumizi yake na kusimamiwa na sheria madhubuti

No comments:

Post a Comment