Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuhusu Mzani
wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao umekamilika kwa asilimia
99.8.
Mzani wa Kisasa wa Vigwaza kama
unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa haraka zaidi kwa muda wa
sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya sasa inayotumia dakika
moja na nusu mpaka mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akihutubia
wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya kuukagua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa Chalinze
Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya
Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.


No comments:
Post a Comment