KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 4, 2015

BONDIA OMARI KIMWERI AMPIGA TAFU YA VIFAA KOCHA SUPER D


Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. kushoto bondia Omari Kimweri na kocha wa kimataifa wa mchezo wea masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakiwa na glove walizo mkabidhi kocha huyo mda mfupi kabla ya kupanda ndege na kurudi kwao



Na Mwandishi Wetu
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi nchini Australia amempiga tafu ya vifaa vya kufundishia kocha wa kimataifa wa mchechezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
wakati wa zihara yake ya wiki mbili ya kutembelea nyumbani kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu zitumiwazo na mabondia wa nje
kabla ya hapo bondia huyo aliongea na wadau mbalimbali wa masumbwi wakati wa mchezo wa ngumi za kulipwa kati ya Iddi Bonge na Alphonce Mchumiatumbo mpambano uliofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kumvalisha mkata wa ubingwa bondia wa uzito wa juu Mchumiatumbo baada ya kuibuka na ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza siku hiyo pia alimpiga tafu kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kwa kumkabidhi vifaa vipya vya kufundishia mchezo wa masumbwi.
Akizungumza baada ya kumkabidhi vifaa kocha Super D alisema amekumbuka nyumbani kwa kuwa ndio alipo zaliwa na kitovu chake kimezikiwa hapa nchini hivyo ataendelea kuwakumbuka zaidi kwa kuwawezesha mabondia kucheza mara kwa mara pindi atakapoanzisha Kimweri Promotioon itakayoshilikiana na Super D Boxing Coach And Promotion kwa kushilikiana kuwapatia mabondia kupigana ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea kipato pamoja na kupandishe rekodi zao kwa mabondia chipkizi
Naye  kocha Super D alishukulu kwa kukabidhiwa vifaa hivyo ambavyo vitamsaidia kuendelea kuinua mabondia mbalimbali chipkizi.

No comments:

Post a Comment