Katibu wa Madereva Mboka akiongea na wandishi wa Habari muda huu, kabla ya mabomu hayajarindima
…Mgomo wa Mabasi kuwa endelevu hadi watakapo achiwa viongozi wao wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Modewji
blog ambayo imepiga kambi katika kituo cha Mabasi Ubungo kuanzia majira
ya saa 11, alfajiri, ni kuwa tayari baadhi ya viongozi wa madereva
wametoa tamko rasmi kuwa mgomo wao huo utaendelea hadi hapo viongozi
wao wakuu zaidi ya Sita (6) wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi
watakapoachiwa huru ikiwa ni pamoja na kuondoa masharti dhidi ya
waliyowekewa katika suala la leseni kwa madereva hao.
Kwa
mujibu wa Katibu Mwenezi wa madereva, Mboka Mwalaikwe alibainisha kuwa
suluhu pekee kwa kunusuru abiria waendelee na safari ni kwa Jeshi la
Polisi kuwaachia huru viongozi hao wanaowashikilia.
“Huu
sio mgomo bali ni kueleza kwamba baadhi ya mambo wanayotufanyia
Serikali sasa yamefika mwisho, Aprili Mosi mwaka huu tulitaangaza rasmi
kuwa ifikapo Aprili 10, endapo madai yetu ya msingi hayajatatuliwa basi
tutagoma.




No comments:
Post a Comment