![]() |
| Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof Tom Mbwete
akitoa neno la shukurani Mkoani Katavi wakati wa hafla fupi ya kuagwa
na wanafamilia wa Chuo hicho tawi la Mkoa wa Katavi katika Hafla
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi ameshauri
Uongozi wa Chuo Kikuu Huria tawi la Mkoa wa Katavi kuwa wabunifu katika
kutafuta vyanzo vya mapato kuliko kutegemea Ada ya wanafunzi na ruzuku
ya serikali katika kujiendesha kuliko kutegemea pato moja tu ambalo
ni ada ya wanachuo.
Ametoa rai hiyo wakati akihutubia Jumuiya ya wananchuo na
wananchi waliofurika kwenye ukumbi wa chuo hicho kwa ajili ya kumuaga
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof,Tom Mbwete aliyemaliza muda wake
kukiongoza chuo hicho. na sasa anakwenda kuhudumia maeneo mengine
katika nchi za Bara la Afrika.
Dkt Msengi amesema uongozi wa Chuo Kikuu Huria Mkoani humo
utumia fursa zilizopo katika Mkoa kuhakikisha wanakuwa wabunifu kupata
vyanzo vya mapato,ambapo wamepata eneo la kujenga Chuo akashauri
waweke miundo mbinu itakayoasaidia kukiingizia chuo mapato kama kujenga
kumbi kubwa zitakazotumika kwa ajili ya mikutano mbalimbali,pamoja na
kumbi za semina kwa wanafunzi ,na pengine watu kutoka nje wanaweza kuja
kukodisha na kuweza kukiingizia Chuo mapato.
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo hicho |
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi katikati anayefuatia kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania aliyemaliza muda wake akibadilishana mawazo na Viongozi wa Mkoa wa Katavi wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo hicho mjini Mpanda. |




No comments:
Post a Comment