Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuvikemea vyombo
vya dola vinavyomfuatafuata vikihoji mambo binafsi na kwamba akishindwa
kufanya hivyo itakuwa wazi kwamba yeye ndiye anawatuma.
Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo jana,
Gwajima alisema amekuwa akifuatwafuatwa na vyombo vya Serikali utadhani
yeye si raia wakati ni Mtanzania halisi.
“Rais Kikwete tafadhali namuomba awakemee watu
hawa... asipowakemea, basi kanisa langu litajua kwamba yeye ndiye
anayewatuma,” alisema Gwajima huku akishangiliwa na waumini waliokuwa
wakimsikiliza.
Huku wakinyeshewa na mvua, waumini hao walikuwa
wakimsikiliza Askofu Gwajima, siku tatu baada ya kiongozi huyo kuhojiwa
kwa mara ya pili na polisi na kutakiwa awasilishe mambo 10 yanayohusiana
na usajili wa kanisa, uongozi na mali zake.


No comments:
Post a Comment