
Dar es Salaam. Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kila mwanachama anapaswa kuwaunga mkono wagombea watakaopitishwa na chama hicho katika nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwani kinyume chake ni kukisaliti na adhabu yake ni kufukuzwa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira alisema
mwishoni mwa juma kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi
Mkuu, chama hicho kinahitaji nguvu za pamoja.
“Sisi bado hatujajiunga na Ukawa, hivyo wanachama
wetu wanapaswa kulitambua hilo na kuepuka kushiriki kwenye ushawishi wa
kufanya kampeni za wagombea wa vyama vingine. Hata kwenye katiba yetu
tunasema sasa tunalenga zaidi katika kujiimarisha ili kutoa ushindani
mzuri wa kisiasa katika uchaguzi huu,” alisema.
Katiba ya ACT, imeeleza wazi kuwa pamoja na sababu
nyingine na kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu,
mwanachama yeyote ambaye atasaidia kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la
kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati chama kimeweka mgombea wake
kwa mujibu wa sheria za nchi, atakuwa amepoteza uanachama wake.


No comments:
Post a Comment