KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 7, 2015

HITMA YA MAREHEMU MZEE KARUME.

B2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
B8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha  hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
B11
Balozi Ali Karume (Mtototo)  kwa niaba ya familia akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha  hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
B13
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
B14
Baba Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba dua wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]                                                 

No comments:

Post a Comment