KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 1, 2015

KUTOKA UTT-AMIS: LEO TUNAZUNGUMZIA USALAMA WA UWEKEZAJI NDANI YA UTT-AMIS

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS Daud Mbaga akitoa maelezo kwa Mbunge kuhusu huduma mbalimbali za UTT-AMIS mjini Dodoma hivi karibuni.

Katika makala yetu haya,Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS Daud Mbaga, anajibu swali kuhusu usalama wa uwekezaji ndani ya UTT-AMIS.




Swali: Faida hizi za uwekezaji ni kubwa sana, je usalama wa mwekezaji ukoje?

Jibu: Kwanza kabisa uwekezaji katika mifuko hii ni uwekezaji mseto.Kuna msemo wa kiswahili unaosema usibebe  mayai yote kwenye kapu moja,hii ikimaanisha uchukue tahadhari maana ukipata ajali yotee yatapasuka.Hivyo hivyo katika mifuko yetu tunaitumia falsafa hiyo ipasavyo. Kiasi fulani cha fedha za mfuko huwekezwa katika hisa, na kiasi kingine katika akaunti za muda maalumu, hati fungani za serikali na hati fungani za kampuni binafsi, pia fedha huwekezwa katika amana nyingine za  uwekezaji katika benki. Iwapo mdororo unatokea sehemu hizi haziwezi kuathirika sawa na hivyo kuendelea kumhakikishia mwwekezaji usalama wa fedha zake, faida shindani na ukwasi wa hali ya juu iwapo atahitaji fedha zake sawa na masharti ya mfuko husika.

Pia UTT- AMIS kama meneja mwendeshaji wa mifuko inadhibitiwa na mamlaka ya masoko ya mitaji na fedha.Vilevile muundo wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni kielelezo tosha cha usalama wa  mali ya mwekezaji ambapo kuna mtoa mtaji ambaye ni serikali ya Tanzania,pili  mtoa mtaji hutoa meneja mwendeshaji ambaye ni UTT- AMIS.Pamoja  na meneja mwendeshaji huwa kuna mwangalizi wa mali ya mfuko ambaye kisheria lazima iwe ni benki ya kibiashara.Mwangalizi wa  mifuko yetu ni CRDB Bank ambaye ana majukumu ya kuhakikisha meneja wa mfuko anafuata taratibu za uendeshaji na uwekezaji  wa mali za mfuko kama ilivyokubalika  katika waraka wa toleo la uwekezaji.Pia kuna uwazi wa hali ya juu ambapo meneja wa mfuko hulazimika kutoa bei ya dhamani ya kipande cha mfuko kila siku za kazi ili iwe rahisi kwa wawekezaji kufuatilia mwendendo wa uwekezaji wao.Taarifa hizi huchapishwa kwenye magazeti na pia hupatikana  katika wavuti yetu. tatu kila mwaka kuna mkutano mkuu amabapo wanachama hukutana na meneja (UTT-AMIS),kupitia taarifa na kutoa mapendekezo mbali mbali.

No comments:

Post a Comment