KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 1, 2015

KUTOKA WAKALA WA VIPIMO (WMA):SERIKALI KUPITIA WAKALA WA VIPIMO YAHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA BORA ZA VIPIMO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza  na Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Magdalena Chuwa alipotembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani hivi  karibuni      
                                                 
Leo katika Makala yetu haya kutoka Wakala wa Vipimo (WMA),Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bi.Magdalena Chuwa anazungumzia Mizani kwenye huduma mbalimbali,fuatana naye hapa chini.....


Anasema Wakala pia una mikakati endelevu ya kuhakikisha kwamba vipimo katika mizani ni sahihi na mara kwa mara maofisa wa  Wakala wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mizani ili kuhakikisha ina toa vipimo sahihi kwa mujibu wa sheria.

Anazitaja mbinu mbalimbali ambazo baadhi ya wauzaji wa wanaotumia mizani wamekuwa wakizitumia kwa  lengo la kuwaibia wananchi.
Mbinu hizo ni pamoja na kutumia mawe yenye uzito pungufu,kutumia mizani yenye muundo usiokubalika kisheria,kutumia mizani au mawe yasiyokuwa na muhuri wa Serikali.

Nyingine ni kuchezea mizani kama vile, kutegua pini, kunatisha nyama kwenye sahani,kuweka sumaku,kufunga uzi kwenye beam ya mizani upande wa sahani,kutumia kisu kuinua mizani upande wa mawe, kufungulia feni upande wa sahani,kutumia na vitu visivyoruhusiwa badala ya mawe kama vile majani ya chai n.k....tutaendelea kesho.
        

No comments:

Post a Comment