![]() |
| Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi 2015 ambao umefikia asilimia 4.3 leo jijini Dar es salaam. Kushoto niKaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja. |
![]() |
Waandishi wa Habari wakiwa
kazini, Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati Mkurugenzi wa Sensa naTakwimu
za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa
taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa
mwezi Machi 2015.
Picha na Veronica Kazimoto – Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Na. Veronica Kazimoto, Takwimu.
Dar es salaam.
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi 2015 umeongezeka
kidogo hadi kufikia asilimia 4.3 ikilinganishwa na asilimia 4.2 za mwezi
Februari kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo
mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa ya mfumuko huo leo jijini Dar es salaam,
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.
Ephraim Kwesigabo amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na badiliko la
bei ya bidhaa na huduma kati ya mwezi Machi na Februari 2015.
Amesema bei ya vinywaji baridi na bidhaa za vyakula ikiwemo
Mchele, Ungawa Muhogo, nyama, Samaki, Maharage, Choroko na Sukari kwa
mwezi Machi imeongezeka kidogo ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi
Februari.
Amesema Mfumuko wa Bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi
umeongezeka kwa asilimia 0.7 mwezi Machi ikilinganishwa na ongezeko la
asilimia 1.6 za mwezi Februari huku Fahirisi za bei kwa mwezi Machi
zikiongezeka hadi 155.88 kutoka 154.83 za mwezi Februari, 2015 kutokana
na ongezeko la bei ya mchele, Samaki, matunda aina ya machungwa,
maharage, mboga mboga na sukari.
Akitoa ufafanuzi kuhusu uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania
katika kununua bidhaa na huduma kwa mwezi Machi 2015 amesema kuwa
umepungua na kufikia shilingi 64 na senti 15 ikilinganishwa na shilingi
64.59 za mwezi Februari 2015.
Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa
mwezi Machi kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema una mwelekeo
unaofanana Uganda ikiwa na Mfumuko wa Bei wa asilimia 1.90 kutika
asilimia 1.4 za mwezi Februari huku Mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa
mwezi Machi 2015 ukiongezeka hadi kufikia asilimia 6.31 kutoka asilimia
5.61 za Februari.
|




No comments:
Post a Comment