Mahmoud Ahmad,Arusha
Joto la ubunge katika jimbo la
Simanjiro mkoani Manyara limezidi kushika kasi mara baada ya mkuu wa
wilaya ya Kakonko,Peter Toima kutamka ya kwamba endapo wakazi wa jimbo
hilo watamshawishi na yeye kushawishika basi atafanya uamuzi mgumu wa
kuchukua fomu kwa niaba yao muda ukiwadia.
Toima,alitoa kauli hiyo hivi karibuni
wakati alipozungumza na Fullshangwe katika jiji la Arusha ambapo
alisistiza kuwa amekuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa makundi
mbalimbali wilayani humo ya kumtaka achukue fomu ya ubunge mwaka huu.
“Kama watu wa Simanjiro wakifanikiwa
kunishawishi na nikashawishika ,nitatii sauti yao na nitafanya uamuzi
kwa niaba yao muda ukiwadia’alisema Toima
Alisema kuwa mara kwa mara amekuwa
akijiuliza ni kwanini wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakimtaka achukue
fomu ya kuwania ubunge wa jimbo hilo na kusema amebaini chanzo
kinatokana na wao kuchoshwa na uongozi uliopo kwa kuwa hakuna
mabadiliko.
Alisema kuwa anasubiri muda ukifika
atafanya maamuzi magumu kwa kuwa kitendo cha wakazi hao kumpelekea
maoombi hayo ni mapenzi yao na msukumo wao ili kukidhi mahitaji yao.
“Watu wa Simanjiro wanatamani kwamba
ningekuwa mbunge wao mimi nasema hayo ni mapenzi yao,msukumo wao ili
kukidhi mahitaji yao”alissiitiza Toima



No comments:
Post a Comment