Madereva
wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo
wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa
Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama
barabarani.
Hali
ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa
wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya
Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku
daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.
Uongozi
wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili
kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni,
kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo
watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.
Waendesha
Bodaboda jijini Dar wakitembelea maeneo ya Vituo vya Daladala kuchukua
abiria Baada ya Daladala kuingia katika Mgomo leo.
Wengine leo walipaga humu ili waendeleaa na shughuli zao za kila siku, maana daladala hakuna kabisa leo jijini dar.
Kituo Kipya cha Sinza ni Cheupeeeeeee....
Daladala za leo zilikuwa ni hizi, hapo ukiwa na buku mkononi unafika safari yako.KWA HISANI YA MICHUZI BLOG






No comments:
Post a Comment