Mshindi
wa mwingine wa milioni 100/- katika promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamis Khalidi (30) mkazi wa mkoani
Mtwara na mjasiriamali anayeuza vifaa vya saluni za kike leo
amekabidhiwa
fedha zake katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambako
amefungua akaunti.
Promosheni
ya JayMillions inayoendelea ikiwa inakaribia kufikia mwisho mnamo
Aprili 23, 2015 imekwishawawezesha baadhi ya wateja wa Vodacom kuwa
mamilionea kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha
kuwa murua na hadi kufikia sasa wamekwishapatikana washindi wawili wa
milioni 100/-, washindi wanne wa milioni 10/- na washindi 39 wa milioni
1/-. Maelfu ya wateja pia wamejishindia muda wa maongezi.
Washindi
wa milioni 100/- ni Uwezo Madegenge kutoka wilayani Kilolo mkoani
Iringa na Hamis Khalidi ambaye amekabidhiwa kitita alichojishindia.
Washindi wa milioni 10/- ni Zuena Rajabu mkazi wa Segerea , Hyness
Petro Kanumba kutoka Rukwa, James Mangu (Mwanza), na Deborah Stanley
mkazi wa Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa shilingi milioni
100 wa promosheni hiyo, Hamis Khalid, amewaomba Watanzania kutambua
mchango mkubwa unaofanywa na Vodacom Tanzania katika kujenga
na kuimarisha maisha ya Watanzania.
"Nimefuatilia
Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha Watanzania
hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama
vile; wamachinga, mama ntilie, na pia wastaafu ambapo
kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa matabaka haya wanahitaji msaada ili
kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari
wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha,"
alisema Khamis.
Aliongeza kuwa yeye ni mfano dhahiri wa Watanzania kuwa promosheni hii haina ujanja bali ya kweli kwa kuwa pamoja na kuishi mkoani ameweza kushinda na leo ameingiziwa fedha zake kwenye akaunti. "Sasa nimepata mwanga katika maisha yangu baada ya kujishindia fedha hizi kwa sababu sijapewa masharti wala utaratibu wowote wa matumizi ya fedha hizi, maisha niliyokuwa nayo yalikuwa ya kuhangaika sana kutokana na kuwa na mtaji mdogo na sasa yamewezeshwa na promosheni hii’’.Alisema.
Khalid
alisema kwa fedha hizi alizojishindia anaona tayari ameanza safari ya
kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio kwa kuwa ataimarisha
biashara yake na kufungua miradi mbalimbali ikiwemo kusaidia familia
yake ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.
Aliongeza
kuwa ana matarajio ya kutoa msaada katika vituo vya watoto yatima kama
njia yake ya kutoa shukrani kwa ushindi huu ambao umebadilisha maisha
yake.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo,
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania
Rosalynn Mworia
aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya JayMillions ili
wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda
namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.
Aliitaja
njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544
iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi
300/- tu.
“Tunaendelea
kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao
zimeshinda hasa kipindi hiki ambacho promosheni inaelekea ukingoni. Kama
Khalid asingetuma ujumbe siku ile angeendelea
tu na maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake
ilichaguliwa kushinda kwa maana bado kuna mamilioni ya kushinda
yanayoweza kubadilisha maisha ya wateja wetu,” alisema Mworia.
Mbali
na kumkabidhi zawadi yake nono hiyo, kampuni ya Vodacom inamsaidia
Hamis kupata mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya ili
kumuwezesha kufanya matumizi yenye tija.
|
| Mshindi
wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto)
mkazi wa Mtwara akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo
cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia)
baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia
promosheni hiyo hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo
Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
|
| .Mshindi
wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto)
mkazi wa Mtwara akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo
cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia)
baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia
promosheni hiyo hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo
Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
|
| Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa Mtwara akikabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mlimani city jijini Dar es Salaam. Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544. |
| Rosalynn Mworia ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania (kulia) akimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi) mkazi wa Mtwara wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544. |


No comments:
Post a Comment