![]() |
| Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bihawana mkoani Dodoma,
Joseph Mbilinyi akizungumza na mwandishi wa Mwananchi kuhusu mwanafunzi
wa kidato cha tano shuleni hapo, Rashid Mberesoro (kulia) ambaye
anahusishwa na tuhuma za ugaidi nchini Kenya. Picha na Sharon Sauwa
Kwa ufupi Habari zilizothibitishwa
na wazazi wake ni kuwa mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya
Sekondari ya Bihawana, Dodoma, baada ya kufaulu katika Shule ya
Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro.
Moshi/Dodoma. Mtanzania aliyekamatwa Kenya akidaiwa kufanya ugaidi
katika Chuo Kikuu cha Garissa uliosababisha vifo vya watu 148, Rashid
Charles Mberesero (20) ni mwanafunzi wa kidato cha tano, lakini uongozi
wa shule anayosoma umesema alitoweka shuleni hapo Desemba mwaka jana. Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kuwa mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana, Dodoma, baada ya kufaulu katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro. Mama mzazi wa kijana huyo, Fatuma Ali alisema jana kuwa: “Baada ya kufaulu alichaguliwa kujiunga na Sekondari ya Bihawana na likizo alirudi nyumbani na baada ya likizo kuisha aliniaga anarudi shuleni.” Taarifa hizo zimekuja wakati Mberesero maarufu kwa jina la Rehani Dida, akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi baada ya watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani juzi. Mwendesha mashtaka, Daniel Karuri alisema, “Rehani Dida” hakufikishwa kortini kwani alikuwa na wapelelezi mjini Garissa kukusanya ushahidi zaidi, baada ya kukiri kuwa ni mfuasi wa kundi la Al-Shabaab. Mtanzania huyo anadaiwa kukamatwa baada ya kujificha kwa saa nane akiwa amejichanganya na maiti, lakini baadaye alipanda na kujificha darini akiwa na mabomu. Kauli ya wazazi Jana, mama huyo, aliliambia gazeti hili kuwa haelewi ni nani aliyemshawishi mwanaye kujiunga na kundi hilo na kwamba jambo hilo limemshtua. |
April 9, 2015
MTANZANIA ANASWA KWENYE UGAIDI WA KENYA "GARRISSA ATTACK"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment