KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 3, 2015

ASKOFU GWAJIMA AFUNGULIWA KESI YA JINAI NA MKAZI WA DAR


Na Mwanishi Wetu 
Mkazi wa Kiluvya, wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani Abubakar Yusufu, ,amemfungulia kesi  ya jinai polisi Askofu wa Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima kilalamika kukwazwa na lugha iliyotumiwa na Askofu Gwajima dhidi ya Askofu Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo.Duru za Kipolisi zainasema
Jana Askofu Gwajima alifika katika kituo Kikuu cha Polisi Jijini Dar es Salaam akitumia baskeli ya magurudumu matatu, lakini polisi waliahirisha kumuhoji hadi tarehe 9 mwezi huu wakiamini afya yake inaweza kuwa imeimarika. 
Jana Askofu huyo hakuzungumza chochote badala yake Mallya ndiye aliyezungumza kwa kifupi na waandishi.  
Mallya alisema Askofu Gwajima amefunguliwa mashtaka ya jinai yanayohusisha kutumia lugha kumkashifu Kardinali Pengo. 
Alisema Yusufu alifungua mashtaka hayo kutokana na picha ya video aliyoiona kwenye mitandao ya kijamii inayomuonyesha Askofu Gwajima akitumia lugha ya matusi kumkashifu Askofu Pengo ambayo kisheria ni kosa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment