Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la
kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani
Afrika Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum
ya Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo
Gweru Bulawayo.
Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka
na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda
kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata
ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum
itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za
Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.


No comments:
Post a Comment