========= ========== ===========
Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imesema itaendelea kudhibiti matumizi ya mtandao katika kuhakikisha hayatumiki vibaya kwa watumiaji.
Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu wakati wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa,Jijini Dar es Salaam. Makungu amesema kuwa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imepitisha sheria ya matumizi ya mitandao katika kulinda ili kulinda matumizi hayo yasitumike vibaya na kuharibu sura ya nchi.Amesema kuwa tafiti mbalimbali za mitandao zimeanza 2010 hali ambayo zinaendelea na kufanya hivyo itasaidia nchi kupata maendeleo katika sekta ya mawasiliano. Naye Mratibu wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasilino,Profesa Benson Nindi amesema kuwa wanaufanya mradi huo katika suala zima la kutoa elimu juu ya utumiaji wa mitandao na serikali ya Tanzania inatakiwa kutunga sera ambayo itasaidia wananchi kwenda kasi na teknolojia ya habari na mawasiliano.


No comments:
Post a Comment