UKWASI wa Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Alliance for Change and
Transparency(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe umeongezeka kutoka umiliki wa
shamba moja na Sh milioni 30 alizokuwa amezihifadhi katika akaunti za
benki mbili tofauti hapa nchini, na sasa anamiliki mali na fedha
zinazofikia Sh milioni 690, MTANZANIA Jumamosi linaripoti.
Kwa mujibu wa taarifa hizo mpya alizoziweka hadharani wiki hii katika
fomu maalum ya kuonyesha mali zinazomilikiwa na viongozi wa chama
hicho, Zitto ametanabaisha kuwa kwa sasa anamiliki nyumba mbili.
Nyumba hizo, moja ina thamani ya Sh milioni 180 na nyingine Sh
milioni 43, Pia anamiliki kitalu cha ekari 12 ambacho kinathamani ya Sh
milioni 25, vyote vikiwa Mwandiga mkoani Kigoma.
Zitto pia ameweka hadharani kumiliki mashamba matatu katika mikoa ya Kigoma, Mtwara na Dar es Salaam.
Katika ufafanuzi wake kuhusu mashamba hayo, Zitto ameeleza kuwa
anamiliki shamba la ekari sita katika manispaa ya mji wa Mtwara likiwa
na thamani ya Sh milioni 60.
Hali kadhalika shamba lingine la ekari tatu lenye thamani ya Sh
milioni 20 huko Matyazo Kigoma, lingine la ekari 3 lenye thamani ya
shilingi milioni 90 ambalo liko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katika fomu hiyo, Zitto alijaza kuwa anamiliki pia gari moja aina ya
Land Lover, Free Lander ambalo alinunua kwa dola za Kimarekani 40,000
sawa na Sh. milioni 72.
Kwa upande wa fedha alizokuwa nazo wakati anajaza fomu hiyo ni Sh.
milioni 18, pia alitanabaisha kuwa amehifadhi fedha katika Benki ya
CRDBNMB na STANBIC zenye jumla ya Sh milioni 9.8.HABARI ZAIDI SOMA MTANZANIA



No comments:
Post a Comment