Pamoja
na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuahirisha tarehe ya kupiga kura ya
maoni, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu na Utamaduni
(UNESCO), kwa kushirikiana na Kampuni ya Focus Media pamoja na Mtandao
wa radio za jamii (COMNETA), limeamua kusambaza Katiba inayopendekezwa
kwa njia ya sauti nchi nzima, ili wananchi wapate elimu kuhusu maudhui
yaliyomo ndani ya Katiba na kufanya maamuzi sahihi pindi siku ya kupiga
kura itakapowadia. Aidha, mkakati huo wa kusambaza Katiba
inayopendekezwa kwa njia ya sauti unajumuisha utoaji elimu kuhusu mfumo
mpya wa kujiandikisha kwa njia ya kieletroniki (Biometric Voters
Registration – BVR) pamoja na kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa
wingi kujiandikisha na kutimiza haki yao ya kikatiba wakati wa upigaji
kura.
Akipokea, nakala za CD zenye
Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti, Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO
nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, alipongeza Kampuni ya Focus Media
kwa kuandaa matoleo hayo na kusisitiza radio za jamii kuzitumia ili
kuwaelimisha wananchi mikoa yote juu ya Katiba inayopendekezwa.
“Nimefurahi sana kuona hizi
nyenzo za kisasa kama SD cards, kwa sababu tunaonesha kwamba radio za
jamii ni njia bora zaidi za kutoa taarifa na pia zinawezesha kupata
mrejesho kutoka kwa wananchi.”
Bi Zulmira Rodrigez, ameongeza
kusema “Hili ni jambo zuri sana kwa jamii, na inapeleka taarifa mpaka
katika njia ya chini kabisa, vijiji vilivyoko ndani kabisa.”
Mwenyekiti wa mtandao wa redio za
jamii Bwana Joseph Sekiku amewashuri watangazaji wa redio mbalimbali
wliohudhuria semina hiyo amewaasa kutumia muda uliobai wa siku28 vizuri
ili kuelimisha jamii maudhui ya Katiba inayopendekezwa ili wananchi
wafanye maamuzi sahihi katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu.
Sekiku ameongeza kwamba kwa sasa
itapatikana kupia Focus Media pro ltd kwa kupitia mitandao yote ya
kijamii na redio mtandao na wananchi wanaweza kuwasiliana kwa kutuma
ujumbe mfupi kupitia namba +255 772 55 55 53



No comments:
Post a Comment