| Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wafanyabiashara
wabainika kukwepa kulipa kodi kwa kuingiza bidhaa kutoka nje kupitia
bandari ya Dar es Salaam, ambapo huandikisha taarifa na maelezo tofauti
na bidhaa halisi zilizomo ndani ya makontena ili kuwawezesha kukwepa
kodi kwa kulipia kiasi kidogo.
Kutokana na udanganyifu huo,
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya alifanya ziara ya kushtukiza katika
bandari kavu Karibu na BP Kurasini jijini Dar es Salaam na kubaini
kuwepo kwa makontena nane yenye bidhaa tofauti na zilizoandikishwa
kwenye nyaraka. Bidhaa zilizokutwa kwenye makontena hayo ni pamoja na
Vitenge pamoja na Vifaa vya kutengenezea pikipiki. Mhe. Waziri wa
fedha vilevile alifanya mshtukizo huo kwa siku mbili ambapo siku ya pili
alishtukiza bandari kavu ambayo ni TRH iliyoko kurasini .Huko aligundua
kuwa waliweka Luninga na Biskuti katika makontena yenye ukubwa wa futi
40 kila moja.
|
No comments:
Post a Comment