…………………………………….
Waandishi wa habari nchini
wameazimia kuboresha Fani ya Uandishi na Utayarishaji wa Vipindi
Vinavyohusu Watu wenye Ulemavu wa Akili ili kuzidi kutetea Maslahi na
Haki za Watu hao.
Maazimio hayo wameyatoa katika
Semina ya Siku mbili ya kuwajengea Uwezo waandishi hao iliyoandaliwa na
Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar (ZAPDD) kwa Msaada wa
Mwenvuli wa Asasi za Kiraia.
Wamesema kuna kila haja ya
kuboresha Habari na Vipindi wanavyotoa kutokana na Jamii ya Watu wenye
Ulemavu wa akili kukumbwa na Changamoto nyingi na hivyo kukoseshwa haki
zao za Msingi.
Aidha wameazimia kuongeza
Ushirikiano wa karibu baina yao na Jumuiya ya ZAPDD ili kuona Jamii hiyo
inawezeshwa kama zilivyokuwa jamii nyingine nchini.
Awali akitoa mada katika Semina
hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Ally Uki aliwataka
Wanahabari hao kuwasaidia Walemavu hao wa Akili kwa kufichua maovu
wanaotendewa ili Jamii ipate uelewa na kulinda haki zao.



No comments:
Post a Comment