WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema
Watanzania waishio ughaibuni hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi
kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa sababu kuna mambo kadhaa ambayo
Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya zoezi hilo kufanyika.
Ametoa kauli hiyo jana jioni
(Jumamosi, Aprili 11, 2015) wakati akizungumza na baadhi ya Watanzania
waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo,
Balozi Peter Kallaghe, yaliyoko Highgate, Kaskazini mwa Jiji la London.
Akizungumza na Watanzania hao
ambao baadhi yao walitoka miji ya Leicester na Manchester, Waziri Mkuu
alisema mambo makuu ambayo yanahitaji kuzingatiwa kabla hawajaweza
kupiga kura ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya
mwaka 1985 pamoja na uandikishwaji wa Watanzania wana-Diaspora kwenye
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.


No comments:
Post a Comment