Tigo Tanzania imetangaza mgao
mwingine wa malipo kutoka kwenye mfuko wa fedha wa Tigo Pesa wenye
thamani ya shilingi bilioni 3.3 (US $ 1.8) kwa wateja wake. Mgao huu wa
fedha ndio wa kwanza katika robo wa mwaka huu.
Malipo haya ni ongezeko la
asilimia 6 ukilinganisha na mgao uliopita wa bilioni 3.1 uliotolewa
katika robo ya mwaka iliyopita 2014. Ongezeko hili linaashiria ukuaji wa
umaarufu wa huduma hii pamoja na ongezeko la idadi ya watumiaji wa Tigo
Pesa, kwa mujibu wa maelezo ya Kaimu Meneja Mkuu, Cecile Tiano.
“Tunayofuraha kubwa
sana tena kutangaza ugawaji wa faida hii kwa watumiaji wetu wa Tigo
Pesa. Malipo haya yanadhihirisha moyo wetu wa kushiriki katika kuboresha
hali za maisha wateja wetu pamoja na nchi zima kwa ujumla,” alisema
Tiano.
Alisema kwamba malipo haya ya robo
mwaka yatalipwa kwa watumiaji wote wa huduma ya Tigo Pesa ikiwemo
mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na mteja mmoja mmoja.
“Tunaamini ya kwamba faida hii ya
robo ya kwanza ya mwaka 2015 itatoa nafuu ya kifedha kwa mamilioni ya
wateja wa Tigo kutokana na mahitaji na matumizi yao waliyonayo,”
alisema.
Meneja Mkuu alielezea, kama
ilivyokuwa awali ya kwamba wastani ya kiwango amabacho mteja atajipatia
itatokana na kiwango ambacho atakuwa alikuwa anakihifadhi katika akaunti
yake ya Tigo Pesa.
Tigo Pesa ilikuwa huduma ya kwanza
ya kifedha ya simu ya mkononi duniani kulipa mgao wa faida kwa wateja
wake pale mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ulipozinduliwa kutoa migao yake ya
fedha rasmi mwezi Julai 2014. Mgao unaofuata war obo mwaka wa fedha wa
mwezi Aprili mpaka Juni 2015 utalipwa mwezi Julai mwaka huu, kutoka na
maelezo ya Meneja Mkuu.
Mgao wa faida kutoka mfuko wa
fedha wa Tigo Pesa inaenda sambamba na tangazo la Benki Kuu lilitolewa
mwezi Februari 2014. Mpaka sasa kampuni imekwisha lipa kiasi cha
shilingi bilioni 23.9 kwa watumiaji wa Tigo Pesa katika migao minne
tofauti ya robo mwaka tangu kuzinduliwa kwa huduma hii Julai 2014.
No comments:
Post a Comment