KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 29, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI WA FIFA LEO, BLATTER ATOA WITO WA UMOJA

Blatter
 Rais wa FIFA Sepp Blatter ametoa wito wa umoja miongoni mwa wajumbe wa mkutano mkuu wa FIFA unaofanyika leo.

Mkutano huo unategemea kumchagua Rais wa FIFA, mchakato wa uchaguzi umetawaliwa na tuhuma kubwa za ufisadi ndani ya FIFA 

Juzi maofisa saba wamekamatwa katika hoteli nchini Uswis. 

Blatter,ambaye anatarajiwa kushinda awamu ya tano ya uongozi. Alisema "Ninatoa wito wa umoja na kufanya kazi kwa moyo kama timu ili tusonge mbele pamoja." 

"Hatuwezi kuacha heshima ya mpira  kupakwa matope" aliwaambia wajumbe wa Mkutano huo . 

Alisema kadhia hiyo inawahusu wale wanaolengwa na uchunguzi wa Wamarekani na mamlaka za Uswiss na si kwa taasisi yote.

Blatter ametakiwa kuachia ngazi lakini amesema wazi kuwa hausiki na tuhuma hizo na binafsi ana nia ya kupiga vita ufisadi.

Katika hatua nyingine, ofisi ya kupambana na ufisadi ya nchini Uingereza imedai kuwa inao ushahidi unaohusiana na kadhia hiyo.

Changamoto

Wanachama 209 watapiga kura kumchagua Rais wa Fifa, Blatter, (79), anapambana na  mwana wa ufalme wa Jordani Ali bin al-Hussein (39).
Katika duru ya kwanza, mgombea anatakiwa kupata 140 kura - mbili ya tatu ili kusinda ili kushinda moja kwa moja

Blatter, amehudumu Fifa kwa miaka 17 anajivunia uungwaji mkono,  kutoka mabara ya Asia, Amerika na Afrika.
Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Nigeria Amaju Pinnick, aliiambia  BBC kwamba ana uhakika Blatter atapata kura 50 dhidi ya 54 za Bara la Afrika.


No comments:

Post a Comment