Picha inayoonyesha taswira ya Burundi
Vyama vya upinzani katika mji mkuu wa Burundi vimesimamisha mazungumzo na serikali kupinga kuzorota kwa usalama baada ya mauaji kiongozi wa upinzani, Zedi Feruzi, Bujumbura, Burundi.
Burundi iko kwenye mgogoro mkubwa kutokana na maamuzi ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania awamu ya tatu ya Urais sanjari na jaribio la mapinduzi lililoshindwa mapema mwezi huu.
Viongozi wa upinzani wanasema wanasitisha mazungumzo na serikali ya Nkurunzinza." Hatuiwezi kuendelea kuzungumza wakati kuna vitisho na mauaji," anasema Pacifique Nininahazwe, mmoja wa wanaharakati.
Muendelezo wa machafuko.
Kiongozi wa upinzani Feruzi,
aliuawa na watu wenye silaha juzi akiwa pamoja na mlinzi wake.
Siku moja kabla, watu watatu waliuawa na wengine 21 walijeruhiwa kutokana na mlipuko wa makombora sokoni.
Wiki iliyopita, Rais Nkurunziza alishinikizwa umoja wa mataifa kusimamisha uchaguzi baada ya ma.andamano hayo,alisogeza uchaguzi kwa siku 1o.
No comments:
Post a Comment